Thursday, 6 January 2011

 
BREKING NEWS: SERIKALI YAINGILIA KATI MZOZO WA KISIASA ARUSHA


Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsi Vuai Nahodha akiongea nasi muda mfupi uliopita. Kulia kwake ni Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema. Picha na John Bukuku

Serikali leo imependekeza pande zinazosigana katika siasia mkoani Arusha kukaa meza moja na kutafuta suluhu kwa mazungumzo na sio kwa vurugu.

Hayo yamesemwa mchana huu na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsi Vuai Nahodha alipoongea nasi ofisini kwake jijini Dar, akiwa na Inspketa Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema, ikiwa ni siku moja baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa CHADEMA baada ya kufanya maandamano yanayodaiwa kuwa si halali. Inasemekana watu wawili wamepoteza maisha na sita wamejeruhiwa vibaya katika vurumai la jana.


Mh. Nahodha, ambaye kabla ya wadhifa wake wa sasa alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibra kwa muda mrefu na kuwa kiongozi mwenye uzoefu wa mambo hayo, amesema serikali imeamua kuingilia kati mgogoro huo kwa kuziweka meza moja pande mbili zinazokinzana ili kuleta amani mpya na kuidumisha jijini Arusha.


Pia Mh. Nahodha amesema askari polisi yeyote ambaye itathibitika alikwenda nje ya mipaka yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waliandamana jana jijini Arusha wakielekea uwanja wa NMC ambako walikuwa wana mkutano wa hadhara. IGP Mwema alikuwa ameshatoa tangazo jana yake (juzi) kwamba maandamano yamezuiwa na yakifanyika ni batili.


Juhudi za kumpata tena Mh. Nahodha kwa ufafanuzi zinaendelea, kwani kuna shauku ya kujua kwamba baada ya serikali kuingilia kati mgogoro huo unaotokana na sakata la uchaguzi wa Meya wa Arusha uliokwamba, je wana CHADEMA waliosomewa mashitaka leo watafutiwa kesi zao?
 
NEWS ALERT: VIONGOZI WA CHADEMA WATINGA MAHAKAMANI JIJINI ARUSHA LEO
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe (pili kulia), Katibu mkuu wa Chama hicho,Dr. Willbroad Slaa (kati) pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini,Mh. Philemone Ndesamburo wakiwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha leo kusomewa mashtaka ya kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano yaliyofanyika jana mkoani humo.
Viongozi wa CHADEMA Wakimsikiliza wakili wao walipokuwa katika Mahakama ya Arusha leo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Willbroad Slaa akipena mikona na baadhi wa wanachama wa chama hicho waliofika Mahakamani hapo kusikiliza hamta ya kesi ya viongozi wao.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, katibu mkuu wa chama hicho Mh. Wilbroad Slaa na wabunge wa Moshi Mjini na Arusha mjini Mh. Philemon Ndesamburo na Goodluck Mrema wamefikishwa mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomewa mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano.

Timu ya Jamii iliyoko eneo la tukio inaeleza kwammba wah. Mbowe, Slaa na Ndesamburo walifika mahakamani hapo kwa pamoja katika gari la kawaida, wakati watuhumiwa wengine wote walifikishwa kwa karandinga.

Hivi tunavyoongea mchakato wa kuwawekea dhamana unaendelea na tutafahamishana kadri habari na picha zitavyokuja toka Arusha.

No comments:

Post a Comment