CHENGE AHUKUMIWA FAINI YA LAKI 7 LEO TU !
awamu ya tatu Andrew Chenge, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
au faini ya Sh 700,000 na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambapo
aliwasilisha faini hiyo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa leo
asubuhi.
Akitoa hukumu hiyo jana Hakimu Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi
hiyo Kwey Rusema alisema uamuzi huo wa Mahakama unafuatia kukamilika
kwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote mbili katika kesi
hiyo iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minane.
Akisoma ushahidi wa awali Rusema alisema Chenge anashitakiwa kwa
makosa manne yakiwamo kuendesha gari bila uangalifu, kusababisha vifo
vya wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine na Victoria Geogre,
kuendesha gari kwa uzembe na kuharibu pikipiki aina ya bajaj pamoja na
kuendesha gari lilikuwa na bima iliyokwisha muda wake.
Katika ushahidi wa awali Chenge aliukana na upande wa mashitaka ambapo
waliitwa mashahidi sita kati yao wanne walikuwa Askari Polisi akiwamo
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu.
Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulidai tarehe 26 Machi 2009 majira
ya usiku wa manane Chenge akiwa katika matembezi yake binafsi alikuwa
anaendesha gari lake aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili
T512ACE kwenye barabara ya Haille Selasie Oysterbay jijini Dar es
Salaam aligonga bajaj na kusababisha ajali iliyosababisha vifo vya
wanawake wawili.
Maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo kuhusu kuendesha gari kwa uzembe
na kuharibu bajaj Chenge aliyakana na kwa madai kuwa alikuwa katika
mwendo wa kawaida kati ya kilo mita 30 hadi 50 na kudai kuwa dereva wa
bajaj alimfuata upande wake kwani yeye alikuwa upande wa kulia zaidi.
Hukumu hiyo ambayo ilitakiwa kusomwa Desemba 16, mwaka huu,
iliahirishwa baada ya Hakimu kukubali ombi la Wakili wa Chenge
aliyeomba kuahirishwa kwa hukumu hiyo kwa kuwa mteja wake alipata
udhuru.
Mponda alidai kuwa mshitakiwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa
kuwa alisafiri kwenda Mwanza kwenye msiba na kuiomba Mahakama
kuahirisha hukumu hiyo.
Kwa mara ya kwanza, Chenge alifikishwa mahakamani hapo Machi 28, 2009
akikabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kuendesha gari kwa uzembe
na kusababisha vifo vya wanawake wawili, kuharibu pikipiki ya matairi
matatu pamoja na kuendesha gari lisilokuwa na stika ya bima.
Katika ushahidi wake mahakamani hapo, Chenge ambaye ni Mbunge wa
Bariadi Magharibi, alidai kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka,
Fortunatus Musilimu, ana ugomvi naye.
Chenge alidai shahidi huyo ambaye aliwahi kutoa ushahidi kuwa mabaki
ya ubongo wa marehemu yalikutwa kwenye gari la Chenge na kuwa
aliwasilisha bima batili, kuwa ni mwongo na ana ugomvi naye.
Ilidaiwa kuwa Machi 27, mwaka jana katika Barabara ya Haile Selassie
Oysterbay, Chenge akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick Up lenye
namba za usajili T512 ACE, aliigonga pikipiki ya matairi matatu
(bajaj) yenye namba T736 AXC na kusababisha vifo vya Beatrice
Costantino na Vick George.
No comments:
Post a Comment