SHUKURANI NA TANGAZO LA MISA KWA MWALIMU KAYUZA
Ilikuwa ni masaa, siku mpaka leo hii umetimiza mwezi mmoja toka ulipotutoka Baba yetu mpendwa MWALIMU JOHN CHARLES KAYUZA. Familia inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshiriki katika kumuuguza na baadae kwenye msiba wa mpendwa wetu aliyefariki tarehe 02/12/2010 saa 2:02 Asubuhi katika hospital ya Mama Ngoma Mwenge na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni tarehe 04/12/2010.
Shukrani za pekee ziwaendee:
1. Madaktari na wauguzi wote wa Hospital za Muhimbili, Ocean Road na Mama Ngoma.
2. Mapadri na wahudumu wa makanisa ya Anglican Mwenge na Temeke.Kwa huduma za kiroho na kushiriki katika Mazishi.
3. Uongozi na wanafunzi wa Alpha High School kwa misaada yao wakati wa ugonjwa na baadae katika mazishi..
4. Uongozi na wafanyakazi wa TAA, St Augustine’s EnglishMedium na ATCL kwa misaada yao na kushiriki kwenye mazishi.
5. Na wengine wote ambao washiriki kwa namna moja au nyingine katika kufariji kipindi chote cha msiba ni vigumu kumtaja kila mmojakwa majina. Kwa niaba ya familia za kayuza, Muya, Samatta, Ntemo,Chilewa, Chilimo, Mattaka na Poyo tunasema asante sana na mungu atazidi kuwabariki.
Unakumbukwa sana na mkeo Edna Muya Kayuza, wanao Josephine, Masauko, Hellen na Simon, Mkweo Japhet Mwaisupule, Augustino na wajukuu zako Gave na Kipesile.
Unakumbukwa pia na wanafunzi wako wa TSJ, Alpha High School na kwingineko kote ulikofundisha
Misa ya kumuombea Marehemu JOHN CHARLES KAYUZA itakuwa siku ya Ijumaa tarehe 07/01/2011 saa 10 jioni katika kanisa la Anglican la watakatifu wote, Temeke , Dar es salaam nakufatiwa na mkesha nyumbani kwa marehemu Temeke Wailes.
Nyote mnakaribiswa.
Bwana alitoa bwana ametwaa, Jina la bwana liimidiwe.
Amin.
No comments:
Post a Comment