THIS WAS THE STORY OF JIPANGUSEE 2010
Lili Kim akiwahamasisha wakazi wa jiji la Dar waliofurika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club katika tamasha la Fiesta Jipanguse,tamasha ambalo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a Mfalme wa raha kamili .

Lil Kim na densa wake wakilishambulia jukwaa

Lil Kim kumbe yuko fiti,anakwenda mpaka chini halafu juu tena.! Watu weweeee..! Mara shemeeejiiiiii.

Juma Nature akijiachia na Lil Kim jukwaani usiku huu

Ni full kujipangusa tu usiku huu.

Lil Kim baada ya kupiga songi zake kadhaa,alimuita msanii Juma Nature jukwaani na kuanza kuimba nae,ama kwa haki kuliibuka makelele na mayowe ya shangwe ile mbaya uwanjani hapa usiku huu.

Daaa mpaka dakika hii naposti picha hizi watu ni wengi sana hapa uwanjani,bado wana hamu ya kuendelea kujipangusa mpaka machweee.

Lil Kim na densa wake wakionesha umahiri wao wa kucheza na jukwaa mbele ya mashabiki wao.

Lil Kima akikamua mbele ya umati mkubwa ndani ya viwanja vya Lidaz usiku huu kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010.

Lil Kim na wapambe wake wakilishambulia jukwaa

Mwanamuziki kutoka nchini Marakani Lil Kim akiingia jukwaani kwa staili ya aina yake iliyowavutia wengi uwanjani hapa isiku huu ndani ya tamasha Fiesta Jipanguse 2010.

Wasanii kutoka NIgeria,Smash na Vast wanaounda kundi la Bracket wakilishambulia jukwaa usiku huu.

Watu kibao ndani ya viwanja vya lidaz club usiku huu wa maneno.

Kikosi cha aldji aladji jukwaani kikitumbuiza.

Mkali wa aladji aladji kutoka Ivory Coast,Jeff akimchezesha densa wake na kibao chake maarufu kabisa cha aladji mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye tamasha la fiesta jipanguse usiku huu ndani ya viwanja vya lidaz club.

Kundi la Wanaume TMK,Chege,Themba na Kr Mulla wakilivamia jukwaani vyema kabisa na moja ya wimbo wao wa Mambo bado,Makelele yametawala hapa uwanjani ile mbaya ni full kujipangasa huku mfamle wa raha kamili akiendelea kutumika safi kabisa.

Mwenyekiti wa Prime Promotions Ltd,Juhayna Ajmi akiwa na baadhi ya Wadau wengine wakifahamiana usiku huu,huku shoo ikiendelea.

Wadau wakijiachia vilivyo usiku huu mara baada ya kunogewa na songi moja kutoka kwa wanaume TMK.

Mafataki kibao yamefyatuliwa usiku huu,shangwe na makalele ya watu kila mahali yakisikika

Wanamuziki wa kundi la Bracket wakiwa na shabiki wao wakiwarusha vilivyo wakazi wa jiji la Dar usiku huu.

Washabiki wakishindana kucheza wimbo wa alaadji jukwaani.

Wadau mpaka sasa bado ni usiku mwingi na watu wako kibao ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinodoni jijini Dar kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,mpaka sasa bado wasanii kibao wamekwishapanda jukwaani na wengine wanasubiri zamu yao wakamue,mashabiki bado wako live ile mbaya.Kumbuka tamasha hili linaletwa kwenu kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti.

Shaa akiwaimbisha washabike wake usiku huu ndani ya viwanaj vya Lidaz kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse linaloendelea hivi sasa,Kinondoni jijini Dar.Kwa hakika watu ni wengi sana na ni kama vile hapatoshi hivi.

Msanii Shaa akiimba singo yake ya Shoga huku akipigwa tafu na madensa wa THT usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club.

Mkali mwingine wa hip hop anaekuja kwa kasi hapa Bongo,Roma akikamua jukwaani usiku huu

Msanii Mataluma kutoka THT na wimbo wake wa Mama Mubaya

Mwasiti akiimba wimbo wake wa Kisa Pombe jukwaani usiku huu

Wasanii mahiri kutoka THT,Barnaba na Lina wakilivamia jukwaa huku wakiwa wamezungukwa na baadhi ya madensa,ama kwa haki usiku umenoga ile mbaya,shangwe kila kona ile full kujpangusa.

Full nyomi Lidaz Club hapatoshi kabisa usiku huu

Msanii wa THT na wimbo wake wa robo saa akiimba jukwaani na madensa wake

Wasanii kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,viwanja vya Lidaz Club kinondoni jijini Dar.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond akiwa katikati ya watu akiwaimbisha wimbo wake Mbagala huku shangwe zikiwa zimetawala kila kona.

Mmoja wa wasanii w a kundi la Offside Trick akihamasisha washabiki usiku huu na wimbo wao wa bata

baadhi ya wadau wakijiachia taratibu usiku huu huku wasanii wakipishana juu ya steji kwa makamuzi ya kufurahisha kabisa bila kusahau makelele ya shangwe kila kona.

Msanii wa muziki wa hip hop aka bongofleva Izzo Bizzness akiwaimbisha washabiki na wapenzi waliofurika usiku huu ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse,viwanja vya lidaz club Kinondoni jijini Dar

Watangazaji wa Clouds FM,B Dozen,Dj Fetty na Adam Mchomvu wakilianzisha jukwaani usiku huu

Baby J akijiachia jukwaani huku mashabiki wakipiga mayowe ya nguvu.

Watu kibao ndani ya Lidaza Clubu usiku huu,huku wasanii mbalimbali wakiendelea kukamua kwa zamu,mashabiki wako live i le mbaya.

Ni full kijipangusa tu usiku huu,kila mmoja kwa mtindo wake huku mfalme wa raha kamili akiendelea kudumisha raha zaidi.

Wwoooowwwww..!

Ni shangwe miluzi na makelele kwa kwenda mbele hapa lidaz club,wadau mapicha yanakuja kila baada ya muda kuwahabarisha kila kinachojiri humu ndani ya viwanja vya lidaz club,watu ndio kama uonavyo wamefurika ile mbaya,suala la vinywaji Serengeti hilo wamelidhibiti vilivyo,msosi ndio kama kawa kila kitu kipo hapa ndani.
No comments:
Post a Comment