
Sehemu ya Logo ilivyokuwa ikionekana kwenye scrini wakati wa uzinduzi

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Entertainment Joseph Kusaga akizungumza jambo usiku wa kuamkia leo wakati wa uzinduzi maalumu wa nembo a.k.a Logo ya Clouds TV pamoja na mchakato rasmi wa kuzianza mbio za tamasha la Fiesta 2010 lenye kauli mbiu ya
Jipanguse Kiserengeti rrhaaaa raaaahhh.,Tamasha hilo linaanza kurindima kesho mkoani Morogoro katika uwanja wa Jamhuri,kiingilio kimepangwa kuwa ni buku mbili kwa kila kichwa.Mdhamini mkuu wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Seregeti .

Bw.Joseph Kusaga akiwashukuru wageni waalikwa kwa kufika kwao kwenye uzinduzi huo usiku wa kuamkia leo katika kiota cha maraha cha Bilicanas,wengineo pichani ni baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa nembo ya Clouds TV.

Mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Entertainment Ruge Mutahaba akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Entertainment Joseph Kusaga kuzungumza machache mbele ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo.

Mmoja wa viongozi waandamizi wa Clouds Entertainment,Sheba Kusaga akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi maalumu wa nembo a.k.a Logo ya Clouds TV pamoja na mchakato rasmi wa kuzianza mbio za tamasha la Fiesta 2010.


Baadhi ya watangazaji wa Clouds TV wakitambulishwa mbele ya wageni waalikwa

Hussein Machozi akiwatumbuiza wageni waalikwa.

Msanii Keisha kutoka kundi la Tip Top Conections

Lina kutoka THT

Diamond na full swagga jukwaani

Diamond akiimba wimbo wake wa mbagala mbele ya wageni waalikwa

Baadhi ya wageni waalikwa kwenye usiku wa uzinduzi maalumu wa nembo a.k.a Logo ya Clouds TV pamoja na mchakato rasmi wa kuzianza mbio za tamasha la Fiesta 2010.

Baadhi ya wasanii kutoka THT wakitumbuiza kwa umahiri mkubwa wageni waalikwa waliofika kwenye maalumu wa nembo a.k.a Logo ya Clouds TV pamoja na mchakato rasmi wa kuzianza mbio za tamasha la Fiesta 2010.
No comments:
Post a Comment