Saturday, 10 July 2010

Dr. Shein Mshindi Dodoma - Halmashauri Kuu


Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM
File

Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalumu cha Halmshauri kuu ya CCM mjini Dodoma
Dr.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Dr.Ali Mohamed Mohamed shei kuchaguliwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma

Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Picha na Freddy Maro

Dr. Shein achaguliwa na Halmashauri Kuu kuwa mgombea Urais wa Zanzibar

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma jana usiku.



Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM .


Baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM wakiwa katika kikao maalum kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment