Thursday, 31 March 2011

 
Wakati natoka Kinondoni nikiwa na braza Mwana FA tukirudi nyumbani tuliweza kuishuhudia ajali hii ikienda kuligonga basi ambalo lilikuwa likuvutwa na basi lingine maeneo haya ya FAO mbele kidogo na Victoria.
Kama unavyoiona bajaji imepiga sehemu ya nyuma ya basi hili ambalo lilikuwa limesimama bila kuonyesha alama zozote za barabarani na kusababisha abiria na dereva wa bajaji hiyo kuumia vibaya.

Dereva wa kibajaji hicho akijaribu kutoka huku damu zikiwa zinamtoka nyingi sana maeneo ya usoni kwake na alivyoshuka alikuwa akichechemea kuashiria amepata majeraha kwenye miguu yake.

Moja wa abiria akiwa analia baada yakupata maumivu kwenye kichwa na miguu yake, alikuwa na mwenzake lakini alikataa nisimpige picha

Dereva wa kibajaji hicho kama unavyomuona akisindikizwa na wasamaria wema akipelekwa kwenye gari ili kukimbizwa hospital

Ilifika mda jamaa alishindwa kutembea maana maumivu yalimzidi kwenye miguu, hadi naondoka hapo dakika 20 zilizopita sikuweza kupata majina yao na wala kujua wameelekea hospital gani kwa matibabu.

Onyo kwa madereva: Kama unaona umepata matatizo usiku basi weka alama zile za barabarani ili anayekuja nyuma yako ajue kuna kitu kimetokea mbele yake, kwa maana huyu dereva wa bajaji nadhani taa yake haikuweza kuona mbali alichokishtukia ni kulivaa gari hilo kwa nyuma na kusababisha hayo yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment