Friday, 24 September 2010

SERIKALI YAZINDUA USAJILI WA WAGANGA WA TIBA ZA ASILI NCHINI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bi. Blandina Nyoni akiwaonyesha wadau mbalimbali na wataalam wa Tiba za asili vitabu vyenye mwongozo wa kuzingatia katika utoaji wa huduma leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Blandina Nyoni akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili Dkt. Ahmad Darusi kuhusu namna ya kutumia Dawa aliyoitengeneza yenye uwezo wa kuwasaidia wagonjwa wa UKIMWI wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bi. Blandina Nyoni akituma fomu za usajili wa waganga wa tiba za asili na tiba mbadala kwa njia ya mtandao katika mikoa yote ya Tanzania leo jijini Dar es salaam fomu ambazo zitapatikana kwenye ofisi za Halimashauri kote nchini kwa ajili ya usajili. Wanaoshudia Kulia ni Mganga mkuu wa serikali Dkt. Deo Mutasiwa na Msajili wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala Dkt. Paul Muhani (Kushoto).
Kiongozi wa kundi la Mjomba Band Msanii Mrisho Mpoto (kulia) akighani mashairi yanayotoa onyo kwa waganga wa tiba za asili wanaotoa huduma kwa wananchi bila vibali na Usajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wataalam wa Tiba za asili wakiwa na dawa mbalimbali za asili walizozitengeneza tayari kwa maonyesho leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Wadau wa tiba za asili na Tiba mbadala wawaliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee leo Jijini Dar es salaam wakifuatilia masuala mbalimbali.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment