Friday, 24 September 2010

filamu mpya ya black Sunday yazinduliwa usiku Wa Leo jijini Dar
Mkurungenzi wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava akimpongeza nyota mmojawapo wa filamu mpya iliozinduliwa usiku wa leo iitwayo Black Sunday,ndani ukumbi wa cinema wa Mlimani City,Steven Kanumba kwa kuonyesha umahiri wake mkubwa wa kuigiza ndani ya filamu hiyo iliokuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji. Mbali ya Kanumba pia kulikuwepo na nyota wengine walioinogesha filamu hiyo vyema kama vile Aunt Ezekiel,Monalisa,Yusuph Mlela na wengineo.Uzinduzi wa filamu hiyo uliandaliwa na kampuni ya Pili Pili Entertainment na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Nyota wa filamu ya Black Sunday iliozinduliwa usiku wa leo,Steven Kanumba akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo iliokuwa na waigizaji wenye vipaji kibao, mara baada ya kutoka kuitazama.
Wageni waalikwa wakiingia kwenye ukumbi kuishuhudia filamu hiyo usiku huu.Kwa picha mbalimbali za tukio hili

No comments:

Post a Comment