Thursday, 15 July 2010

Lindsay Lohan atumia mistari ya 50 Cents kuwajibu wapinzani wake.

Wakati zikiwa zimebaki siku tano kabla ya kuanza kutumikia kifungo chake cha gerezani. Pop star Lindsay Lohan ametumia mistari ya kiongozi wa kundi la G-Unit 50 Cents kujitetea kutokana na kifungo cha siku tisini alichohukumiwa hivi karibuni, Hatua hiyo imekuja baada ya watu kumsema vibaya, super star huyu ndipo alipoamua kuazima line za 50 Cents, si kwa kuimba kwenye nyimbo…

no no no…… mwanadada huyu ametumia mistari hiyo kwa kuandika kupitia Twiter, ….kabla hatuja endelea…unaweza uka guess ni line gani za 50 alizotumia na zinatoka kwenye ngoma gani? na album yenyewe inaitwaje?


Niskize mimi….


Album inaitwa Get Rich or Die Tryin, ngoma inaitwa "Patiently Waiting."


Line zenyewe ni kama ifuatavyo, 'You shouldn't throw stones if you live in a glass house and if you got a glass jaw, you should watch yo mouth," Kwa kiswa kingi inakuwa kama ifuatavyo:- hutakiwi kurusha mawe wakati unakaa kwenye nyumba ya kioo, kama una taya la kioo unatakiwa uwe makini na mdomo wako,


ndivyo alivyo andika mwanadada Lindsay Lohan mwanzoni mwa wiki hii kupitia Twiter, kama nilivyosema mwanzo hiki ni kijembe kwa wale walio msema na wanao endelea kumsema vibaya, Lohan alihukumiwa kifungo cha siku 90 jela kutokana na kitendo chake cha kupuuza masharti ya kifungo cha nje, kisheria inaitwa Violeting probation, kwa kushindwa kuhudhuria darasa la kupinga matumizi ya Vileo, kama alivyoamriwa na mahakama.

Lindasy anatarajiwa kuanza kifungo chake tarehe 20 mwezi huu, yaani jumanne ijayo… pole sana dada tuko pamoja na wewe katika wakati huu mgumu kwenye maisha yako, ….jela sio mchezo muulize T.I.D

No comments:

Post a Comment