NITAFANYA”-KIDUM Ft.LADY JAYDEE
Mapenzi bila visa na mikasa ni mapenzi yaliyokosa chachu.Ni kama vile maisha yasiyo na kupanda wala kushuka.Yanakosa msisimko au kwa kizungu wanasema ‘boring”.Lakini inakuwaje kama visa na mikasa katika mapenzi baina ya wawili yanakuwa yamejaa visa vya kudanganyana,kunyanyasana,kutoheshimiana? Mbaya zaidi ni kwamba visa na mikasa hiyo haina mapumziko.Kila kukicha kuna msala mpya.Ukiambiwa usamehe utakubali?Ukiambiwa vumilia tu utakubali?Ukipewa ahadi kwamba “nitajaribu” kufanya au kuwa sahihi utaiamini?
Maudhui kama hayo ndiyo yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa mwanamuziki maarufu Jean Piere aka Kidum kutoka nchini Burundi akishirikiana na mwana wa kwetu,Lady JayDee au ukipenda Judith Wambura.Wimbo umesimamiwa na Hermy B kutoka B’Hits Music Group ambaye hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi na Kidum ingawa ameshafanya kazi kadhaa na Lady JayDee zikiwemo nyimbo Mtarimbo Doro na Teja. Usikilize hapo chini.
No comments:
Post a Comment