Saturday, 8 May 2010

AJALI YA KUSIKITISHA YATOKEA VIGWAZA....MAGARI MATATU YAMEUNGUA NA MAISHA YA WATU YAMEPOTEA

Haya ni mabaki ya mifupa ya binadamu alieungua mpaka kuisha kabisa baada ya gari lililokuwa limebeba mafuta kugonga gari jingine na kusababisha moto

Mafuta yaliomwagika toka kwenye gari



Askari wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio




Gari yenye container ilipaki baada ya kuwa na hitlafu, kwahiyo utingo wake akashuka kwenda chini ya uvungu wa gari ku cheki nini tatizo.
Ndipo gari la mafuta lilitokea kwa nyuma bila kuwaona likagonga kwa kishindo.

Gari jeupe lililopo kushoto dereva wake aliziona gari zote hizo mbili kabla ajali haijatokea, akajisalimisha kwa kuitumbukiza gari yake katika msitu kama mnavoiona..

Mlipuko wa moto ulipotokea uliteketeza gari ya mafuta iliogonga gari lililobeba container na kusababisha moto huo kufikia kuunguza magari yote matatu.
Jambo linalosikitisha ni pale ajali ilipotokea yule utingo aliekuwa uvunguni mwa gari lililobeba container alibanwa akashindwa kutoka, aliomba watu wamuokoe kwa kumkata mikono iliokuwa imebanwa ili aweze kujinasua...lakini raia walishindwa kufanya hivyo mpaka moto ukamfikia na kumteketeza kabisa huku akijiona

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7 za usiku, tar 6

No comments:

Post a Comment