
Msichana mmoja huko nchini Nigeria ameripotiwa kufariki dunia baada ya kukatwakatwa na mapanga na mtu aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa siku nyingi.Tukio hilo limetokea baada ya mrembo huyo kuanzisha mahusiano mapya na kijana mwingine raia wa Marekani kwa njia ya mtandao wa facebook ambapo penzi liliponoga walikuwa wakikutana hotelini nchini Nigeria ambako kijana huyo huwa anaenda kwa ajili ya kukutana na mrembo huyo.Lakini baadae mpenzi halisi wa mrembo huyo ambae walipanga kufunga nae ndoa aligundua mchezo huo na siku walipopanga kukutana tena
hotelini hapo,mchumba wa marehemu ambaye pia ni raia wa Nigeria alivamia hotelini hapo na kuanzisha ugonvi,lakini baadae waliporudi nyumbani
ndipo mrembo huy alipomtamkia waziwazi kwamba yeye hamtaki tena.Siku chache baadae baada ya kutamkiwa hivyo kijana huyo alimteka mpenzi wake huyo na kutokomea nae na baadae ikagundulika kuwa alimkatakata kwa mapanga hadi kifo chake.( majina ya wahusika wote hayakuweza kupatikana kutoka kwenye chanzo chetu cha habari)
No comments:
Post a Comment