TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2011 LATEKA HISIA ZA WENGI USIKU HUU,SHANGWE NA MILUZI YALINDIMA KILA KONA.
Mwanamuziki Ludacris akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye viwanja vya Lidaz Club,ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2011.ambalo kwa sasa limetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake,aidha tamasha hili limeandaliwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions kwa kushirikiana na Clouds FM,huku mdhamini mkuu wa tamasha hilo ikiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Serengeti premium lager.
Luda akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu.
Watu walikuwa kibao,halafu shangwe kila kona na miluzi ya haoa na pale ilitawala usiku.
Ludacris akikamua jukwaani usiku huu.
Pichani shoto ni Mwanamuziki Ludacris sambamba na mwanamuziki mwenzeke wakianza kulishambulia jukwaa usiku huu,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,ambalo linatimiza miaka 10 sasa,tangu kuanzishwa kwake.
Dj wa Mwanamuziki Ludacris akiwema mambo sawa,kabla ya Luda kupanda jukwaani.
Umati wa wati ukifuatilia kilochokuwa kikiendelea jukwaani usiku huu.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akiendeleza ukongwe wake jukwaani pichani kati,huku baadhi ya wasanii wenzake wakimpa tafu akiwemo mwanadada machachari kabisa,Dayna
Ana majina kibao msanii huyu,ukimuita Binam kwakwe sawa,ukimwita Mwana FA aaah ndio kabisa,jina lake halisi anaitwa Hamis Mwinyjuma,akionyesha umahiri wake wa kurap jukwaani mbele ya maelfu ya watu waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,kwenye viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu.
Mmoja wa wasanii nyota katika miondoko ya Hip hop hapa Bongo,Fd Q akitumbuiza jukwaani mbele ya maelfu ya watu waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,kwenye viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu.
Mandojo na Domokaya wakizikumbushia enzi zao jukwaani.
Msanii mahiri wa Kike kutoka nyumba ya vipaji THT,aitwaye Lina akicheza jukwaa na mmoja wa madensa wake kwa namna ya kipekee usiku huu,ambao shangwe za hapa na pale ikiwemo miluzi kibaoo.
Nyomi la Watu
Kijana mdogo hivi lakini mambo yake ni makubwa awapo jukwaani,anaitwa Beka Boy kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani.
Msanii wa kike Mwasiti pamoja na msanii mwingine anayeibukia vilivyo katika anga ya hip hop bongo,Gozilla wakilishambilia jukwaa la Serengeti Fiesta 2011 usiku huu.
Wakazi wa jiji la Dar ambao wametoka kila kona wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Msanii mwimbaji na mtunzi kutoka THT aitwaye Amin akiwa na kundi lake wakionyesha umahiri wa kucheza jukwaani kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu.
Msanii mahiri wa kizazi kipya Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
Pichani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti Breweries Limited,Tedd Mapunda,Mkurungenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafuru pamoja na Mdau wakiwa wamepozi huku wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea jukwaani usiku huu kwenye viwanja vya Lidaz Clud,Kinondoni jijini Dar.
Umati wa watu uliofurika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,wakishangilia majotro yanayaoendelea hivi sasa,ama kwa hakika ni full kujiachia watu ni wengi na ulinzi upo wa kutosha kabisa.
MAKAMUZI YAMEISHAANZA HIVI SASA NDANI YA VIWANJA VYA LIDAZ CLUB .
Bofya kucheki mpango mzima wa serengeti fiesta 2011 hivi sasa inavyoendelea.
M
sanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Mataluma akitumbuiza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,kwenye viwanja vya Lidaz Club Kinondoni jijini Dar,watu ndio kama hivyo uonavyo mdau,na wengine wanazidi kumiminika tu.
Lidaz hapatoshi kabisa,ni full kujiachia kama kawa na wala haina majotro kabisa.
Haaaaa haaaaaaa majotro mchezo,lazima uende hewani kama mzuka umepanda kama hivi pichani.
Wako standby,lolote likitokea fasta unapewa huduma ya kwanza.
Mapozi ya picha kama kawa tu.
more of the coverage by Jax collection click : http://jaxcollection.blogspot.com/p/gallary.html
No comments:
Post a Comment