Thursday, 17 February 2011

JK akisisitiza wananchi wa rejee wasiwe na hofu na wasisikilize redio mbaowaziri wa ulinzi na wakuu wa vitengo jeshini wakiteta jambochuma kikavu sio isssue sasa masela
Align CenterAfisa wa Msalaba Mwekundu,Mama Jane Lweikiza akiwa amembeba mtoto aliekutwa maeneo ya Sitaki Shari,Ukonga mchana huu kutokana na kutojulikana walipo wazazi wake mara baada ya kutokea kwa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto usiku wa kuamkia leo.Wahanga woote waliokumbwa na mkasa huo wapo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar kutokana na hali ya usalama wa maisha yao pamoja na kupatiwa misaada mbali mbali.
Bw. Salum Madaba wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Mwalimu Kiondo wa Shule msingi Tandika wakimnywesha maziwa mmoja wa watoto waliopo katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar ambaye haijulikani wazazi wake walipo mpaka hivi sasa.
Watu Msalaba Mwekundu wakishusha Maji ya Kunywa kwa ajili ya Wahanga hao waliopo ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar hivi sasa.Misaada mbali mbali inaendelea kuleta Uwanjani hapa ili kuweza kuwasaidia watu mbali mbali waliopo uwanjani humu kutokana na kukumbwa kwa tukio hilo la milipuko ya mabomu katika makazi yao huko Gongo la Mboto na maeneo ya jirani na hapo.
Wengine wakiwa nje ya uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kupumzika chini ya vivuli vya miti kutokana na kutolala usiku wa kuamkia leo kwa hali ya milipuko ya Mabomu iliyotokea maeneo ya Gongo la Mboto katika maghala ya silaha ndani ya kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Mtoto Gerald Samson akiwa na Mareraha usoni mara baada ya kuumia wakati akijaribu kutaka kujinusuru na milipuko hiyo jana usiku.
Kamanda wa Scout akiwapanga vijana wake katika makundi mbali mbali ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar,mchana huu.
Sehemu ya Matenti ya dharula yaliyowekwa ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar.
Hawa ni Watoto ambao waliokotwa huko Gongo la Mboto wakiwa wako peke yako kutokana na wazazi wao kukimbilia sehemu zisizojulikana kutokana na milipuko ya mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto.
Sehemu ya Wahanga wa Mabomu ya Gongo la Mboto wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar wakisubiria kujua nini kinaendelea kwa upande wao.
Baadhi ya watoto wakiendelea kuletwa uwanjani hapa kwa ajili ya mapumziko na kama kuna ndugu wa karibu aweze kuwatambua.
Bado watu wanaendelea kuelekea uwanja wa Uhuru hivi sasa.

Kwa Picha Zaidi

BOFYA HAPA

Vodacom Foundation kusaidia wahanga wa Gongolamboto


Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba ameviambia vyombo vya habari kwamba.

Kampuni yake kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea katika kambi ya Jeshi Gongolamboto Jijini Dares Salaam:Na hivyo kumfanya kuamua maamuzi ya haraka kama yafuatayo.

1. Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15599 kupitia mitandao yote.
Ujumbe huu utatozwa shilingi 1000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga. Red alert itawasha rasmi kesho ijumaa tarehe 18.

2. Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji kwa siku nzima ya ijumaa kwa wahanga zaidi ya 1000 waliopo Uwanja wa taifa ambao wengi wao ni watoto

3. Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga. Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika. Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 0767111403

4. Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi. Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu mbalimbali

Kizaazaa cha mlipuko wa mabomu kambi ya jeshi Gongo la Mboto usiku huu


Majeruhi akifikishwa hospitali ya Amana usiku huu baada ya kukumbana milipuko ya mabomu kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar usiku huu. Bado haijulikani wangapi wameumia ama kupoteza maisha katika milipuko hiyo iliyotokea kwenye ghala ya silaha za jeshi huko Gongo la Mboto na kusikika kila sehemu ya jiji
Daktari hospitali ya Amana akimhudumia mmoja wa majeruhi wengi walioletwa hospitalini hapo
Mmoja wa majeruhi akipata huduma hospitali ya Amana

Deo rweyunga wa Radio One akiongea na
mmoja wa majeruhi hospitali ya Amana

Majeruhi wa milipuko ya mabomu
Watoto wakiwa na mama yao aliyejeruhiwa hospitali ya Amana
Huduma kwa majeruhi
Mdau baada ya kupata huduma ya kwanza hospitali ya Amana
majeruhi akifikishwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Gari la wagonjwa likiwasili Muhimbili usiku huu likiwa na majeruhi wa mabomu hayo
majeruhi wakiwa Muhimbili
Majeruhi akiwasili Muhimbili
Daktari akiwa na mtoto ambaye kapotezana
na wazazi wake hospitali ya Amana

Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa, ankal, askari na Deo rwedyunga wakiwa eneo la tukio kwenye geti la kuingilia kambi hiyo ya Gongo la Mboto ambako raia walizuiwa kuingia
Wakaazi wa Gongo la Mboto na maeneo ya
jirani wakitafuta pa kwenda

Kizaazaa Gongo la Mboto usiku huu
Wananchi wakihaha huku na kule Gongo la Mboto
Mbio mbio kuepusha maafa Gongo la Mboto


No comments:

Post a Comment