MWAKA HUU KAZI KWELI KWELIII.!
WABUNGE WA ZAMANI WAONEKANA KUSHINDWA KUTAMBA
Kwa mujibu ya Matokeo rasmi yaliyotangazwa na wasimamizi wa vituo hivi /husika ni kwamba katika jimbo la Kigoma Mjini mgombea Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha CCM,Bwa Peter Serukamba amembwaga mpinzani wake wa chama cha CHADEMA ,Bwa.Ali Mlee kwa kuibuka na kura 20,594 kwa 19,414.
Wakati huo huo mgombea Ubunge kwa jimbo la Kigoma Kaskazini,Bwa.Zitto Kabwe amemgaragaza mgombea mwenzake wa chama cha CCM,Bw.Robbinson Lembo,ambapo Zitto Kabwe ameibuka na kura 23,500 huku Robbinson akiibuka na kura 18,970.
Kama vile haitoshi huko jijini Mwanza katika jimbo la Ilemela,matokeo rasmi ni kwamba Mgombea wa chama cha CHADEMA,Hyness Willson amembwaga vibaya mgombea wa chama cha CCM,Bwa.Antony Diallo kwa kujinyakulia kura zaidi ya 30,000 dhidi ya Diallo ambaye amepata kura 26870.Nae Bw.Lawlence Masha wa CCM amebwagwa kwa namna ya pekee na mpinzani wake wa CHADEMA Bw.Ezekia Wenje kwa kuibuka na kura 38,131 huku Masha akipata kura 27,883.
Pichani ni Mbunge mteule wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Godbless Lema akiwa anaondoka katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge akiwa anasindikizwa na wanachi pamoja na wapambe wake. Mh. Lema amepata kura 56, 569 dhidi ya Dk. Batilda Burian wa CCM aliepata kura 37,460. Picha na Woinde Shizza wa Globu ya JaX.
Mh. John Magale Shibuda (pichani) na Silvester Kasulumbayi wametangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi kuwa wabunge wa maswa magharibi na mashariki kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu.
Wakati huo huo mgombea Ubunge kwa jimbo la Kigoma Kaskazini,Bwa.Zitto Kabwe amemgaragaza mgombea mwenzake wa chama cha CCM,Bw.Robbinson Lembo,ambapo Zitto Kabwe ameibuka na kura 23,500 huku Robbinson akiibuka na kura 18,970.
Kama vile haitoshi huko jijini Mwanza katika jimbo la Ilemela,matokeo rasmi ni kwamba Mgombea wa chama cha CHADEMA,Hyness Willson amembwaga vibaya mgombea wa chama cha CCM,Bwa.Antony Diallo kwa kujinyakulia kura zaidi ya 30,000 dhidi ya Diallo ambaye amepata kura 26870.Nae Bw.Lawlence Masha wa CCM amebwagwa kwa namna ya pekee na mpinzani wake wa CHADEMA Bw.Ezekia Wenje kwa kuibuka na kura 38,131 huku Masha akipata kura 27,883.
jimbo la arusha mjini lanyakuliwa na gobless lema
shibuda na kasulumbayi watikisa maswa magharibi na mashariki

No comments:
Post a Comment