Friday, 29 October 2010

Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza mazungumzo ya Mheshimiwa Kikwete na waandishi wa habari


Wawakilishi wa TBC Susan Mongy na ITV Masatu wakiwa kwenye mazungumzo na Mheshimiwa Kikwete leo

Awamu ya pili ya maswali ya wawakilishi wa vituo vya televisheni mbalimbali nchini kwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrsiho Kikwete imeanza wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari.

Baadhi ya maswali yaliyoulizwa ni yale kuhusiana na maboresho kwenye sekta ya afya na ahadi za mgombea kwa Watanzania kuhusiana na afya, manung'uniko kuhusu utoaji wa haki katika mahakama, tatizo la rushwa na jinsi mgombea atakavyoendesha mapambano dhidi ya rushwa.

Mwisho Mheshimiwa Kikwete alitoa rai kwa Watanzania wote kutumia nafasi waliyopewa kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka. Pia aliongeza kuwa Watanzania tuna historia ya amani duniani kote haswa kipindi cha uchaguzi. Aliwasihi watanzania kutofuata muelekeo wa kuchagua viongozi kwa misingi ya dini kwani kwa kufanya hivyo, itaweza kuleta migogoro nchini baada ya uchaguzi.

Mazungumzo ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete na waandishi wa habari Leo

Mheshimiwa Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na wawakilishi wa vituo mbalimbali vya televisheni nchini usiku wa leo


Baadhi ya waalikwa wakisikiliza mazungumzo ya baina ya mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM na waandishi wa habari usiku wa leo tarehe 29.10.2010

Mheshimiwa Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa Arnaoutoglou jijini Dar es salaam kuanza mazungumzo na waandishi wa habari leo.

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na waandishi wa habari leo tarehe 29.10.2010


Mazungumzo ya mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na waandishi wa Habari yanaendelea kwenye ukumbi wa Arnautoglou kuanzia saa mbili usiku hadi saa nne usiku.

Baadhi ya maswali yaliyo ulizwa na wawakilishi wa vituo mbalimbali vya televisheni ni:
- Kuhusu mtazamo wake kuhusiana na wizi wa kura vituoni wakati wa upigaji kura.
- Matokeo ya tafiti mbalimbali  zinazoashiria matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010,
- Ajira kwa vijana,
- Maendeleo kwenye sekta ya elimu,
- Halihalisi ya nchi katika mizunguko yake ya kampeni nchi nzima,
- "Legacy" atakayowaachia watanzania pindi atakapomaliza muda wake wa uongozi
- Aliwezaje kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa CCM waliokuwa na kesi mbalimbali na shutuma mahakamani
- Na mwisho ni sura ipi ya serikali atakayoiunda pindi akifanikiwa kuendelea kuongoza ambapo atamuachia kiongozi mwingine tayari kuanza safari ya mwaka 2025 ya malengo ya milenia.

Awamu ya kwanza ya maswali imemalizika, na sasa awamu ya pili ya maswali inaanza.

Mazungumzo haya yanarushwa moja kwa moja na vituo vyote vya televisheni. Pia Radio Clouds na Radio Uhuru wanarusha mazungumzo haya mojakwamoja.

VIZA televisheni ya kwenye mtandao wa internet kupitia HabariCom inarusha mazungumzo haya moja kwa moja kwenye mtandao wa internet, pamoja na kurasa zote za jamii za jakayakikwete2010 (social media sites) za twitter, facebook na blogspot.

Mkutano wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM na Waandishi wa Habari

Mgombea urai wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na waandishi wa habari usiku huu kwenye ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar es salaam leo tarehe 29.10.2010

Mkutano wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na waandishi wa habari unaendelea sasa hivi kwenye ukumbi wa Arnautoglou Mnazimmoja jijini Dar es salaam. 

Mkutano huo unaojumuisha maswali yanayoulizwa na wawakilishi wa vyombo vya habari na kuratibiwa na Bi. Asha Mtwangi, unahusisha vituo tisa vya televisheni vikiwemo ATN, Channel 10, East Africa TV, TBC, TV Milimani, Clouds TV, Star TV na ITV.

No comments:

Post a Comment