waziri mkuu pinda apiga kura kijijini kwake.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi kijijini kwake, Kibaoni, Katavi mapema leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mke wa Waziri Mkuu. MamaTunu Pinda akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi kijijini Kibaoni, Katavi, mapema leo. (Picha na Ofisi ya WAziri Mkuu).
JK na Mama Salma wakipiga kura leo
JK akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga,Chalinze leo asubuhi.
JK akionyesha wino uliopo katika kidole chake ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa keshapiga kura leo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msoga iliopo Chalinze leo asubuhi.DK. Gharib Bilal APIGA KURA KIEMBE SAMAKI

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akionyesha vidole vyake vikiwa na wino baada ya kutoka katika chumba cha kupigia kura kwenye Kituo cha Kiembe Samaki leo.

Mgombe mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura wakati alipofika katika kituo cha uchaguzi cha Kiembe Samaki mjini Zanzibar mapema leo asubuhi.Picha na Muhidin Sufiani.
dk. Salim katika zoezi la kupiga kura mjini dar leo

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim, akipiga kura leo jijini Dar es salaam ya kumchagua Rais , Mbunge na Diwani. Dkt Salim aliwasili katika Eneo la Soko la Samaki Msasani saa 12.50 Asubuhi na kufanikiwa kupiga kura katika Kituo B 3 cha Soko la Samaki Msasani saa 1.30 Asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim akisubiri Kitambulisho chake kutoka kwa Karani wakati Karani huyo akiendelea na uhakiki ili kudhibitisha kama kweli jina lake limo katika daftari la wapiga kura ili aweze kwenda kupata katarasi za majina ya wagombea ili kushiriki zoezi la upigaji kura za kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.
No comments:
Post a Comment