Saturday, 11 September 2010

vuta nikuvute ya fm academia yazinduliwa kwa mbwembwe jijini dar


Mkurugenzi wa Mabibo Heineken Beer Benedicta Rugemalila kulia akiashiria kuzinduliwa kwa albama ya sita "Vuta Nikuvute" ya Bendi ya muziki wa dansi FM Academia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo wakishirikiana kwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Kelvin Twisa wa pili kutoka kulia na Felician Mutta katikati.
Wacheza shooo wa kike wa bendi ya FM Academia wakilishambulia jukwaa kwa staili ya pekee kabisa uliowavutia watazamaji wengi waliofika kuushuhudia uzinduzi wa albamu mpya ya bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Diamond usiku wa kuamkia leo.
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya,Nameless akimbembeleza kwa sauti nzuri huku akiwa amepiga magoti mmoja wa mashabiki wakati alipokuwa akiimba kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo wakati wa uzinduzi wa albamu ya bendi ya FM Academia ijulikanayo kwa jina la Vuta Nikuvute.
Rais wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadaat wa mwisho kulia akiongoza wanenguaji wa kiume kutoka bendi hiyo wakati walipopanda jukwaani kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, FM Academia wanazindua albam yao ya sita inayoitwa "Vuta Nikuvute" usiku wa kuamkia leo.
Ilikuwa ni vuta nikuvute ile mbaya ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee wakati bendi hiyo ilipokuwa ikiizindua albamu yake mpya ya sita ijulikanayo kwa jina la VUTA NIKUVUTE na kuhudhuria na watu kibao waliovutiwa kwa kiasi kikubwa na shoo safi iliyotolewa na bendi hiyo usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment