Saturday, 4 September 2010

Redd's mitindo yafana,miss Redd's kutajwa siku ya kilele cha miss Tanzania 2010

Meneja wa Kinywaji cha Redds Primaim Cold, Kabula Nshimo akiwakalibisha wageni waalikwa usiku kwenye shindano la kumsaka mrembo ataeibuka na taji la Miss Redds 2010 usiku huu ndani ya Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar.

Madizaina wakifuatilia kwa makini tukio hilo
Wanafuatilia kwa makini kabisa
kushoto pichani ni Meneja Mawasiliano wa TBL,Edith Mushi akiwa na wageni waalikwa wkifuatilia kwa makini shindano la kumsaka Miss Redds usiku huu
Wageni waalikwa mbalimbali ndani ya tukio la kumsaka mlimbwende atakaeibuka na taji la miss redds usiku huu.



Kushoto na Kulia Mwisho watoto wa Makao Makuu (Idodomia)


Picha za warembo mbalimbali wapatao 30,ambao watashiriki shindano la Miss Tanzania 2010,ambao pia usiku huu anatafutwa Miss Redds 2o1o ndani ya Mbalamwezi Beach Mikocheni jijini Dar,Wageni waalikwa mbalimbali kibao wakishuhudia tukio hili.Haya wadau mapicha yanakuja kibao endeleeeni kulibarizi jamvi.




Ubunifu wa mavazi wa Asia Idarous wang'ara miss Redd's 2010


Mama bingwa wa mitindo ya mavazi hapa Bongo na kwingineko Mama Asia Idarous Hamsini kutoka Fabak Fashions akiwapunigia mikono wageni waalikwa akiwa ameambatana na walimbwende wa Miss Tanzania 2010,wakiwa wamevalia mavazi yake aliyoyabuni na kuonyeshwa usiku huu kwenye shindano la kumsaka mlimbwende wa taji la Miss Redds 2010 lililofanyika ndani ya Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar usiku huu.

No comments:

Post a Comment