Sunday, 22 August 2010

Ziara ya Vodacom Miss Tanzania KINAPA
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wamebeba mabegi mngongoni mithili ya watalii wanaoteremka mlima Kilimanjarto wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), David Loosurutia (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya mazingira ya hifadhi hiyo kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakati warembo hao walipotembelea KINAPA. Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia michoro ya ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kialimanjaro (KINAPA) wakati warembo hao walipotembelea KINAPA. Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusindikiza watalii kupanda Mlima Kilimanjaro wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro. Warembo hao wapatao 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment