Sunday, 11 July 2010


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakimzingira Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema wakati alipotumi nafasi ya kutoa salamu za chama chake kwa kumwagia sifa tele Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutekeleza kwa ufanisi program mbalimbali za maendeleo nchini, pia alisifia sana uimara wa chama cha CCM na nidhamu ya chama.

Uzuri wa ndege manyoyaaaaa

Uzuri wa CCM seraaaaa

Huu ni ujumbe wa Khadija Kopa akimfagilia Mheshimiwa Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa Chama Cha TLP alipofungua moyo wake akimmwagia sifa kede kede Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete.



Hapa sasa hivi Lyatonga Mrema anatoa salamu rasmi kutoka chama cha TLP na kuwasema wale wanaosingizia katumwa na wana CCM wakome.

Anashangiliwa na wana CCM kwa nyimbo na vigelegele, anasema kwamba CCM haikamatiki. CCM Chama Kubwa, amesalimu amri. Kwani mwaka 1995 alishindwa, mwaka 2000 aligaragazwa na Mh. Mkapa, na mwaka 2005 ndio kabisaa Kikwete akammaliza. Hivyo CCM ni chama imara, hakishikiki. "Kweli CCM inagaragaza upinzani".



Mheshimiwa Mrema aliongeza, "Kila mwaka wa uchaguzi inakula kwangu, sasa nimechoka" anasema Mrema kwa hamasa huku akiendelea kusifia CCM na uongozi wake.



Kwa maneno yake amesema, hana sababu ya kuacha kumsifia Rais Kikwete kwani ndiye Rais pekee anayemjua. Amefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka mitano hususan katika harakati za kupambana na ufisadi na mafisadi nchini.



Amekiri ya kuwa katika marais wengi waliopita, Kikwete ni mthubutu na mtekelezaji. Anaumia roho sana kusikia kuna watu wanaombeza ati hajafanya lolote hivyo wamtose.



Mrema amewasuta wote wanaobeza maendeleo ya serikali ya Rais Kikwete na amewaomba wana CCM waendelee kumsaidia ili afanye vizuri zaidi. Hapo Mrema alishangiliwa sana kwa nyimbo za CCM na kusindikizwa na bendi ya TOT.


Mrema amemaliza kwa kusema ya kwamba anafuata wosia wa baba wa Taifa na hivyo atagombea ubunge vunjo kupitia chama chake cha TLP.


Mwenyekiti wa CCM amemshukuru kwa kuwa mkweli lakini amemuhakikishia ya kwamba hata wana CCM watakwenda huko VUNJO na watakutana tena.


Mambo moto moto hapa Kizota, salamu zinaendelea. Picha zinakuja

Burudani ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM - Kizota, Dodoma

Dokii a.k.a suprise aliimba na kucheza kwa madaha akishukuru CCM kwa kuwapa nafasi vijana kupata nafasi katika chama. Style ya nywele ya Dokii iliwapendeza wengi kwani ilikuwa na rangi za bendera ya taifa - bluu, njano, nyeusi, njano na kijani.
Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili Flora Mbasha na kundi lake zima waliinua mashabiki wengi wa nyimbo za injili na wimbo wao uliokuwa na speed ya kasi na uliowasisimua wengi. Wimbo huo ulisifu uongozi wa Mwenyekiti wa CCM ukisihi kuongeza ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kuleta maendeleo Tanzania.

Kada wa CCM mwanadada Vicky Kamata akitumbumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu na wimbo wake mpya kuhusu uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete.

Wasomaji utenzi kutoka Tanzania visiwani walitunzwa na kuinua wajumbe wengi vitini kwa mpangilio mzuri wa mashairi yao yaliyoisifu nchi ya Tanzania na viongozi wake mahiri.

Baadhi ya vikundi vinavyotumbuiza leo ni Vijana wa CCM Vyuo Vikuu, Tanzania One TOT, Wanaume TMK, Flora Mbasha, Vicky Kamata, na wengine wengi.

Lakini waliofunika na kushangiliwa na umati wa wajumbe wengi ni vijana wa CCM wa vyuo vikuu kwa ujembe wao uliokuwa na vijembe kebekebe kwa wapinzani.

Video clip ya wimbo huu itapanda hewani pindi internet itakapostabilize. Lakini baadhi ya maneno kwenye wimbo wao ni kwamba mikoa yote waliyopita kutafuta udhamini wananchi walisema chaguo lao ni Jakaya Kikwete na CCM. Wanamuasa Jakaya asiwe na hofu hao wapinzani ni kama "mavuvuzela" hayatamzuia kufunga goli la ushindi.

Wageni waliohudhuria Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma






Taswira ya Barabara iendayo Kizota Dodoma ambapo Mkutano Mkuu wa CCM umeanza Leo Asubuhi saa nne.

Wafuatao ni baadhi ya wageni walioalikwa kutoka Vyama vingine vya siasa ndani na nje ya Tanzania.

Matawi yote ya CCM nje ya Nchi : Washington DC, London, India etc

Vyama Kutoka Nje Ya nchi

Chama Cha Kikomunisti cha China - China

Chama Cha SWAPO - Namibia

Chama Cha FRELIMO - Mozambique

Chama Tawala Rwanda

Chama Tawala Botswana

Chama CNDDFDD - Burundi

Chama Cha FLA cha Algeria -

Chama cha Wafanyakazi - Korea

Vyama Pinzani Ndani ya Tanzania: Hawa wote wameshangiliwa sana na wajumbe wote lakini kwa shangwe zaidi walishangiliwa sana Mrema na Lipumba ambapo wajumbe wote walisema CCM.

TLP - Lyatonga Mrema

CUF - Mwenyekiti bara Dr. Ibrahim Lipumba

UMD - Mwakilishi
Na Vyama vingine vingi.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribisha wageni na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM leo Mjini Dodoma.
Jukwaa kuu limepambwa kwa picha za viongozi wakuu wa CCM na kauli mbiu ya Mkutano Mkuu "Pamoja Tuzidi Kusonga Mbele"

Bango la kuwapokea wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM karibu na lango kuu kuingilia Kizota ukumbi ambao Mkutano Mkuu wa CCM unaendelea kwa siku mbili.


Agenda na Ratiba ya Mkutano Mkuu wa CCM - Kizota, Dodoma

- Kufungua Mkutano

- Marekebisho ya Katiba ya CCMya Mwaka 1977 Toleo la Julai 2010

- Taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010

- Uteuzi wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM

- Kufunga Mkutano

No comments:

Post a Comment