Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo cha utii kwa Chama Cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wakati wa maandamano ya kumuunga mkono yaliyofanyika mjini Dodoma.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Kaimu Mwenyekiti UVCCM Beno Malisa, na Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba.
Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma walishiriki katika maandamano ya kumuunga mkono kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Urais mwaka huu kwa tiketi ya CCM.
Baadhi ya vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakiandamana kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua fomku kwaajili ya kugombea nafasi ya urais 2010.
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo mchana.Picha na Freddy Maro.
No comments:
Post a Comment