Friday, 14 May 2010

sean kingstone atinga ndani ya studio za Clouds Fm a.k.a mjengoni

Sean Kingstone akifanya mahojiano mafupi ndani ya redio ya Choice FM na mtangazaji ML Chriss leo jioni,hapa Mikocheni jijini Dar.
Mwanamuziki Sean Kingston na Crew yake wametinga ndani ya studio za Clouds Fm leo jioni
Sean Kingstone akiiimba moja ya wimbo wake ndani ya studio za mjengoni Clouds Fm leo jioni
Sean Kingstone akisalamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kussaga leo jioni alipokwenda kuitembelea kampuni hiyo akiwa ameongozana na Crew yake,Sean kingstone ametua jijini Dar na kesho atakuwepo kwenye utoaji wa tuzo za Kili Music Awards ambayo ni maalum kwa wageni waalikwa tu, na Jumamosi msanii huyo ataangusha bonge la shoo pamoja na wasanii wengine wa hapa nyumbani.
Mwanamuziki Sean Kingstone akiwa ameongozana na bodi gadi wake wakiwasili Mjengoni leo jioni kwa ajili ya mahojiano mafupi
ziara ya Sean Kingston ndani ya kiwanda cha tbl
Crew ya Sean Kingston ikipata ufafanuzi wa namna ya vinywaji vya kampuni ya TBL vinavyotengenezwa,leo jioni mara baada ya kufanya ziara ndani ya kiwanda hicho
Mmoja wa wataalamu wa Kiwanda cha bia TBL akiwaonesha na kutoa ufafanuzi wa namna vinywaji vya TBL vikitengenezwa.
Crew ya mwanamuziki Sean Kingstone ikishuhudia utengenezwaji wa vinywaji mbalimbali ndani ya kiwanda cha TBL.
Mwanamuziki Sean Kingston pamoja na Crew yake wakijichana msosi wa nguvu ulioandaliwa kwa ajili yao leo mchana ndani ya ofisi za kampuni ya bia ya TBL.
Mambo ya mnuso
"Eeeh Sean Kingstone kumbe nae analibeneke la blog"!
Mgeni nae yuko bize kuchukua matukio
Mchuma aliowasili nao Sean Kingstone kwenye ofisi za kampuni ya bia ya TBL pamoja na Crew yake walipokwenda kufanya ziara na kufahamu namna ya vinywaji vya kampuni hiyo vingitengenezwa leo mchana
Sean Kingstone wakielekea kwenye chakula cha mchana walichoandaliwa na wenyewe wao TBL leo mmchana.

Mmoja wa wafanyakazi wa TBL akiwaongoza wageni wake
Sean Kingstone akisain kitabu cha wageni ndani ya ofisi za TBL leo mchana huku Mkurugenzi wa Masoko TBL , David Minja akishuhudia pamoja watu wengine.

Sean Kingstone akishuka taratiibu kwenye ofisi za kampuni ya TBL
Mwanamuziki Sean Kingstone akifunguliwa mlango na bodi wake kabla ya kushuka

Wenyeji wakimsubiri mgeni wao afike

sean kingstone kukamua vilivyo jmos diamond jubilii

Sean Kingstone akiwa ameambatana na bodi gadi wake pichani kulia,wakirejea hotelini mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari mapema leo asubuhi
Eeeh bwana hapa vipi,mie nikiwa nimepigwa konozzz na mkali wa swagazzz Sean Kingstone leo
Mwanamuziki Sean Kingston katikati akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja kushoto na Meneja wa kinywaji cha Kiliamanjaro Premium Lager George Kavishe baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari ,Mwanamuziki huyo yuko nchini kwa mwaliko wa TBL kwa ajili ya kushiriki katika utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards zitakazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Sean KingStone akiteta jambo na Meneja wa kinywaji cha Kiliamanjaro Premium Lager George Kavishe,kabla ya mkutano na waandishi wa habari kuanza mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree,Oysterbay jijini Dar
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Sean Kingstone na Wenyeji waliomleta hapa Nchini Kampuni ya Bia ya TBL,wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi ndani ya hoteli ya Double Tree,Oysterbay jijini Dar kuhusiana na onesho la mwanamuziki huyo wa kimataifa,Sean Kingston atakuwepo kesho kwenye utoaji tunzo kwa wasanii watakaoibuka kidedea na jumamosi atakamua ndani ya ukumbi wa diamond jubilee jijini Dar.

No comments:

Post a Comment