Monday, 9 November 2009

MAISHA CLUB KWISHAAAA ...YATEKETEA KWA MOTO

sehemu kuu ya burudani Maisha Club iliyopo Masaki jijini Dar leo mnamo majira ya saa saba mchana ilianza kuwaka moto, kwa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wamesema kuwa kulikuwapo na ukarabati uliokuwa unaendelea wa vipupwe (AC), kwa bahati mbaya wakati wa ukarabati huo mojawapo ikalipuka kutokana na nyaya zake kugusana, na baadaye moto mkubwa ukazuka katika jengo hilo, imeelezwa kuwa taarifa zilifika kwa watu wa zima moto lakini hawakuwahi kuuzima moto huo kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa vitu vilivyokuwemo vilikuwe vimekwishateketea.

hii ndio ilikuwa sehemu ya kuingilia maishani
sura ya mbele ya club maisha kulia ndipo swiming pool ilipo
maisha club inavyoonekana baada ya kuwaka moto
nini kimesababisha maisha club kuungua leo?
askari wa zimamoto wakipambana na moto uliokuwa unateketeza maisha club ya ostabei jijini dar mapema leo. hakuna aliyedhurika na janga hili ambalo chanzo chake bado kujulikana, japo redio mbao zinataja hitilafu zilizotokana na umeme. moto mtindo mmoja
sehemu yote ya mbele ya maisha club imeteketea

mama hellen sweya, mmiliki wa maisha club, akifarijiwa
mama sweya akiwa hana la kusema, akimuachia Mungu kila kitu

Kikozi cha zima moto kikiwa bize kuuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka
Sehemu ya kuingia ndani ya maisha Club ikiwa dhohofu li hali
Sehemu ya dancing floor ikiwa imeteketea kabisa
Sehemu ya mbele iliyo karibu na swimming pool ikiwa imeteketea kwa moto kabisa
Mmiliki wa kiota cha maraha Maisha Club,Mama Hellen Sweya (kati) akipewa pole na baadhi ya marafiki zake waliofika kwenye eneo la tukio leo jioni Masaki jijini Dar.Kwa picha zaidi bofya

No comments:

Post a Comment