HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ALEX MUKAMA KUSSAGA

Kuzaliwa; Marehemu alizaliwa Julai 7, 1932 katika kijiji cha Bwasi Majita Musoma vijijini.
Masomo;
= Elimu ya Msingi alisoma Bukima Primary school kuanzia mwaka 1942 ambapo alihitimu darasa la nne. Mwaka 1946 alijiunga na Shule ya Mwisenge Middle school ambapo alisoma darasa la tano hadi la nane.
= Mwaka 1951 alijiunga na Chuo cha Ualimu Pasiansi Mwanza na kufuzu cheti cha Ualimu mwaka 1952.
= Mwishoni mwa mwaka 1952 baada ya kuhitimu cheti cha Ualimu alibakizwa hapo chuoni kama mkufunzi. Aliendelea kufundisha Pasiansi Teacher Training Centre hadi chuo kilipohamishiwa Butimba Teacher Training Centre-Mwanza. Alijiuzulu kazi ya ualimu mwaka 1959 na kujiunga na vyama vya Ushirika Ukerewe Growers Corperative Union.
= Mwaka 1961 aliacha kazi ya Ushirika na kuingia Serikali kuu ambapo alipelekwa Mzumbe Institute of administration kusomea utawala. Baada ya kumaliza masomo Mzumbe 1962 aliteuliwa kuwa Local Government Officer kule Njombe District-Southern Highlands Province wakati huo.
= Kwa juhudi na bidii aliyokuwa nayo kazini, mwaka 1964 alipandishwa cheo kuwa Regional Local Government Officer-Southern Highlands Province-Mbeya.
= Mwaka 1965 alihamishiwa Musoma na kuteuliwa kuwa Town Clerk wa mji wa Musoma.
= Mwaka 1967 alihamishiwa mjini Iringa kama Town Clerk, mji ambao ulikuwa mkubwa kuliko Musoma.
= Mwaka 1968 alipandishwa cheo na kuhamishiwa Mwanza kama Town Clerk ambako alifanya kazi hadi mwanzoni mwa mwaka 1973 ambapo alihamishiwa Mtwara Township.
= Akiwa Mtwara, marehemu alijiuzulu kazi za Serikali na kujiunga na Shirika la Bima la Taifa kama Meneja Utawala mwaka 1973 april. Akiwa Meneja utawala Bima, mwaka 1976 alikwenda Uingereza kuchukua mafunzo ya Utawala katika Chuo kikuu cha Manchester.Aliendelea kufanya kazi Bima na kupandishwa cheo kufikia ngazi ya Mkurugenzi wa Utawala Shirika la Bima hadi alipostaafu 1991.
Mzee Alex alishiriki katika uundwaji wa kampuni kubwa ya Media inayoitwa Clouds Entertainment. Kampuni hii ikihodhi baadhi ya makampuni yafuatayo; Clouds fm/choice fm/clouds tv ambapo mpaka kutokea kifo chake yeye akiwa ndiye Mwenyekiti.
Marehemu ameacha mke na watoto tisa, pamoja na wajukuu 11.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
, Amen.Marehemu ameacha mke na watoto tisa, pamoja na wajukuu 11.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe











Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wakiwa wametulia kwa makini wakifuatilia sala iliyokuwa ikiendeshwa kwa ajili ya kumuombea marehemu,Mzee Alex Kusaga.
Ndugu,jamaa na marafiki walifika kwa wingi kanisani kwa ajili kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao Marehemu Alex Kusaga.

No comments:
Post a Comment