New Maisha Club kuzinduliwa!
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EML Francis Anthony Ciza Majey akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa Club maisha mapema leoasubuhi,shoto ni meneja wa club hiyo Allan Ngugi
Moja ya sehemu mbili za Ma DJ
Kila sehemu kumetakataBOFYA HAPA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.
“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.
Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.
“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.
“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.
Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo
ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.
No comments:
Post a Comment