MAISHA CLUB KWISHAAAA ...YATEKETEA KWA MOTO
sehemu kuu ya burudani Maisha Club iliyopo Masaki jijini Dar leo mnamo majira ya saa saba mchana ilianza kuwaka moto, kwa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wamesema kuwa kulikuwapo na ukarabati uliokuwa unaendelea wa vipupwe (AC), kwa bahati mbaya wakati wa ukarabati huo mojawapo ikalipuka kutokana na nyaya zake kugusana, na baadaye moto mkubwa ukazuka katika jengo hilo, imeelezwa kuwa taarifa zilifika kwa watu wa zima moto lakini hawakuwahi kuuzima moto huo kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa vitu vilivyokuwemo vilikuwe vimekwishateketea.
hii ndio ilikuwa sehemu ya kuingilia maishani
sura ya mbele ya club maisha kulia ndipo swiming pool ilipo
maisha club inavyoonekana baada ya kuwaka motonini kimesababisha maisha club kuungua leo?
Sehemu ya kuingia ndani ya maisha Club ikiwa dhohofu li hali
Mmiliki wa kiota cha maraha Maisha Club,Mama Hellen Sweya (kati) akipewa pole na baadhi ya marafiki zake waliofika kwenye eneo la tukio leo jioni Masaki jijini Dar.Kwa picha zaidi bofya



No comments:
Post a Comment